Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) imezindua Ripoti yake ya Uendelevu wa Mazingira, Jamii na Utawala (ESG) ya mwaka 2024, ikieleza miradi mbalimbali iliyotekeleza kwa lengo la kuleta maendeleo endelevu.
Uzinduzi huo umefanyika leo Jumatano Septemba 24, 2025 jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau kutoka sekta binafsi na umma, huku Balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania, Peter Huyghebaert, akiongoza tukio hilo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa TBL, Michele Kilpini amesema kampuni hiyo imeendelea kuwekeza kwenye miradi ya maji safi kwa jamii, kuwawezesha wakulima kupitia mafunzo na pembejeo, pamoja na kuwajengea uwezo wauzaji wa rejareja.